Tafuta ShuleShule.info | Ukurasa wa nyumbani

Karibu katika shule.info. Tovuti hii inatoa taarifa kwa kina na kwa undani zinazohusu matokeo ya mitihani ya Kidato cha Nne 2012. Taarifa hizi zinaweza kulinganishwa kwa mkoa, shule au kwa somo. Taarifa kuhusu matokeoyaliyorudiwa kwa kupangwa upya na kutangazwa mwezi Mei 2013 nazo pia zimejumuishwa

Tunakuhimiza kupitia tovuti hii na kutupatiaa maoni na mapendekezo yako . Tunaichukulia tovuti hii kama zana iliyo hai na tunakusudia kuiongezea ubora na taarifa mpya kadiri siku zinavyosonga mbele. Tunatangaza kwamba data zetu zitawekwa wazi na zinaweza kupatikana kwa kila mmoja huku tukikaribisha msaada, fikra au matumizi yake.

Kufuatiwa kupitiwa upya kwa matokeo ya mwaka 2012, wanafunzi zaidi ya 1,598 walipata Daraja la I na wanafunzi pungufu ya 36,889 walifeli mitihani. Je unataka kujua zaidi kuhusu taathira ya kupitiwa huko upya? Ona mapitio ya 2012

Tangu mwaka 2004 ambapo data zilianza kupatikana, shule iliyofanya vema kabisa kwa ujumla (kwa kuchukua wastani katika miaka yote) ni Shule ya Wasichan ya St. Francis Girls. Je, umpeleke mwanao shule gani? Tembelea shule ili kujua.

Licha ya ukweli kwamba shule mbili zilizofanya vema katika miaka yote hiyo ni za wasichana, bado kuna tofauti katika viwango vya kufaulu kati ya wavulana na wasichana. Lakini tofauti hii inaonekana kupungua. Soma Zaidi ...

Mkoa wa Dar es Salaam una idadi kubwa zaidi ya watahiniwa kuliko mahali pengine ambapo ulikuwa na watahiniwa 41,956 mwaka 2012 peke yake. Lakini bado Dar es Salaam inashika nafasi moja kati ya tano kimkoa (katika mikoa 23) kwa mwaka 2012. Je, hii ina maana kwamba wanafunzi wa Dar es Salaam wanapata mahitaji zaidi? Je, tungetarajia Dar es Salaam iwe ya kwanza? Tembelea ukurasa wa mikoa ili kuona tofauti.

Pata Kadi ya mwanafunzi ya Matokeo

Pata matokeo ya kila mwanafunzi kwa kuingiza mwaka wake wa mtihani, namba ya mtahiniwa na kituo chake cha mtihani.
Mwaka
Namba ya Kituo
Namba ya Mtahiniwa